• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Telkom Kenya yaanzisha huduma ya kutuma pesa kwa simu

  (GMT+08:00) 2018-03-12 19:24:21

  Kamapuni ya mawasiliano Telkom Kenya imezundua huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu ikitoa ushindani kwa kampuni za safaricom na Airtel.

  Kupitia kwa huduma hiyo mpya, Telkom inatarajiwa kujiunga na Safaricom na Airtel kwenye huduma mpya itakayowezesha wateja kutuma na kupokea pesa kupitia kwa mitandao yote .

  Waziri wa Tehama Joe Mucheru anasema serikali iko kwenye msitari wa mbele kusaidia wadau kwenye sekta ya benki simu kufanikisha malengo yao.

  Kenya ilikuwa ya kwanza duniani kuanzisha huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu na sasa kuna zaidi ya wateja milioni 28.2 kwenye huduma hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako