• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michuano ya dunia ya Raga wachezaji 7 kila upande: Kenya yaelemewa na Fiji

  (GMT+08:00) 2018-03-13 08:38:39

  Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya wachezaji saba kila upande ya Kenya imemaliza ya pili katika michuano ya dunia ya Sevens Series baada ya kufungwa katika mchezo wa fainali na Fiji kwa alama 32-12 jijini Vancouver nchini Canada jana asubuhi.

  Fiji ambao ni mabingwa wa michezo ya Olimpiki, wamekuwa wakifanya vizuri dhidi ya Kenya na huu umekuwa ushindi wake wa 34 katika historia ya nchi hizi mbili katika mchezo wa raga.

  Kenya sasa inashikilia nafasi ya nane kwa alama 64 katika msururu wa mataifa yanayoshiriki katika michuano hiyo nyuma ya Uingereza ambayo inashikilia nafasi ya saba kwa alama 70.

  Afrika Kusini inaendelea kuongoza kwa alama 109 huku Fiji ikiwa ya pili kwa alama 101.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako