• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa msaada wa mchele kwa Liberia

  (GMT+08:00) 2018-03-13 08:53:56

  China imetoa msaada wa tani 1,243 za mchele kwa Liberia. Taarifa iliyotolewa jumapili na serikali ya Liberia inasema makontena yote 50 ya mchele yamefika nchini humo na kukabidhiwa kwa maofisa wa serikali ya Liberia. Kaimu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Elias Shoniyin amesema msaada huo uliotolewa kutokana na ombi la serikali ya Liberia, utasaidia kukabiliana na kuongezeka kwa bei ya chakula nchini humo. Balozi wa China nchini Liberia Bw. Fu Jijun amesema msaada huo utafikishwa kwa watu wenye mahitaji, na China inapenda kuisaidia Liberia kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha sekta yake ya kilimo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako