• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu Mkuu UN alaani kushindwa kutekelezwa kwa Azimio la Umoja wa mataifa kuhusu Syria

  (GMT+08:00) 2018-03-13 09:24:46

  Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Antonio Gutteres amelaani kushindwa kutekelezwa kwa azimio la Umoja wa mataifa kuhusu usimamishaji wa vita nchini Syria.

  Akiripoti kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu utekelezaji wa azimio nambari 2401, Bw Guterres amesema uhasama nchin Syria haujakomeshwa. Kwenye baadhi ya maeneo makali ya vita yamepungua, lakini mapambano yanaendelea katika maeneo mengine ya Ghouta Mashariki na zaidi, ikiwa ni pamoja na Afrin, Idlib, Damascus na vitongji vyake.

  Bw. Guterres amesema licha ya kuruhusiwa kwa baadhi ya magari ya kutoa misaada, utoaji wa misaada ya kibinadamu na huduma nyingine si salama, na unakwamishwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako