• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa atoa mwito wa kuondoa ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake

  (GMT+08:00) 2018-03-13 09:25:04

  Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres amesema ni muhimu kubadilisha mambo yasiyo na usawa yanayosababisha ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake.

  Akiongea kwenye mkutano wa 62 wa Kamati ya hadhi ya wanawake duniani ulioanza jana na kufanyika hadi Machi 23, Bw. Guterres amesema, hadhi ya wanawake ni changamoto kubwa zaidi kwa wakati huu, na ni maslahi ya kila mmoja. Amesema ubaguzi dhidi ya wanawake unaharibu jumuiya, mashirika, makampuni, uchumi na jamii.

  Bw. Guterres amesema kwa sasa binadamu tunaishi kwenye dunia na utamaduni uliotawaliwa na wanaume, ndio maana kuna haja ya wanaume wote kuunga mkono haki za wanawake na usawa wa kijinsia.

  Hata hivyo amesema kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia bado ni tatizo, ametolea mfano wa mabalozi katika umoja wa mataifa na kusema asilimia 20 kati yao ni wanawake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako