• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UN kutoa chanjo ya surua kwa watoto milioni 4.7 wa Somalia

  (GMT+08:00) 2018-03-13 09:42:48

  Shirika la Afya duniani WHO, Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF, na wizara ya afya ya Somalia wamezindua kampeni ya kutoa chanjo ya surua kwa watoto zaidi milioni 4.7 wenye umri kati ya miezi sita hadi miaka 10 nchini Somalia.

  Mwakilishi wa WHO nchini Somalia Bw. Ghulam Popal amesema, Kampeni hiyo itaimarisha juhudi za kuboresha kinga dhidi ya surua na kuwafikia watoto wasiopewa chanjo.

  Kwa mujibu wa WHO na UNICEF watoto 2,800 wanaodhaniwa kuwa na ugonjwa wa surua wameripotiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wengi kati yao wanatoka sehemu za Bay, Banadir na Mudug. Mwaka 2017, watu zaidi ya elfu 23 walidhaniwa kuugua ugonjwa wa surua, idadi ambayo ni mara sita kuliko ile ya mwaka 2016, na asilimia 83 kati yao ni watoto wenye umri chini ya miaka 10.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako