• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa UN apongeza maafikiano kati ya rais wa Kenya na kiongozi wa upinzani

  (GMT+08:00) 2018-03-13 09:56:05

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonia Guterres amewapongeza rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na kiongozi wa chama cha upinzani NASA Bw. Raila Odinga kwa kufikia makubaliano ya kufanya juhudi za pamoja katika kuhimiza umoja wa taifa.

  Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Stephane Dujarric amesema Bw Antonio Guterres amepongeza taarifa ya pamoja iliyotolewa tarehe 9 mwezi huu na rais Uhuru Kenyatta na Bw Raila Odinga, ambayo inaonyesha dhamira yao ya kushirikiana kwa ajili ya kuimarisha umoja wa taifa la Kenya.

  Ameongeza kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameahidi kushirikiana na serikali na wananchi wa Kenya katika kuimarisha amani, utulivu na maendeleo nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako