• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Sudan Kusini awafuta kazi waziri wa fedha na ofisa wa jeshi

  (GMT+08:00) 2018-03-13 10:13:07

  Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini jana alimwondoa madarakani waziri wa fedha Bw Stephen Dau na kumteua Bw. Salvatore Garang Mabiordit kuchukua nafasi yake.

  Rais Kiir pia amemwondoa Bw. Marial Chanoung kutoka wadhifa wa mkuu wa operesheni, mafunzo na intelijinsia wa jeshi la ukombozi la watu la Sudan. Bw Chanoung ni mmoja kati ya maofisa sita waandamizi wa serikali na wapinzani, waliowekewa vikwazo na Baraza la usalama la umoja wa mataifa kutokana na kukwamisha mchakato wa amani, na kuzuia usambazaji wa misaada.

  Amri hiyo ya rais iliyotangazwa kupitia radio ya serikali jana jioni, haikutaja sababu za kuwafuta kazi maofisa hao. .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako