• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kazi ya ujenzi wa daraja refu zaidi la kamba barani Afrika yakaribia kumalizika

  (GMT+08:00) 2018-03-13 10:16:29

  Kampuni ya Maputo Sul ya Msumbiji imetangaza kuwa, kampuni ya barabara na daraja ya China imemaliza asilimia 95 ya kazi ya ujenzi wa daraja la kamba juu ya ghuba ya Maputo, Msumbiji ili kuunganisha mji wa Maputo na kaunti ya Catembe.

  Msimamizi wa viwango wa kampuni ya Maputo Sul Bw. Basilio Dzunga amesema, kutokana na kuzihamisha familia za watu wanaoishi karibu na eneo litakalotumiwa kujenga daraja hilo, mradi huo unatarajiwa kumaliza mwezi wa Juni. Amesema, ujenzi wa daraja lenyewe unatarajiwa kukamilika mwezi wa Aprili, ili kuacha nafasi hatua za uhitimisho kama vile kupaka rangi na kufanya marekebisho madogomadogo.

  Habari zinasema daraja hilo litakuwa daraja refu zaidi la kamba barani Afrika, na litarahisisha mawasiliano kati ya watu wanaoishi katika pande mbili za ghuba hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako