• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapongeza Umoja wa Mataifa kwa juhudi zake za kusuluhisha mgogoro wa kibinadamu nchini Syria

  (GMT+08:00) 2018-03-13 16:39:17

  Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ma Zhaoxu amesema, China inaupongeza Umoja wa Mataifa na katibu mkuu wake kwa juhudi zao za kusuluhisha mgogoro wa kibinadamu nchini Syria, na kusisitiza kuwa azimio namba 2401 lazima litekelezwe kihalisi.

  Balozi Ma amesema, tarehe 24 mwezi Februari, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio namba 2401 ambalo limetoa fursa ya kusitisha mapambano. Lakini pande zinazopambana bado zinaendelea kushambuliana, na ushoroba wa kibinadamu ambao umeanzishwa na Russia hauwezi kufanya kazi ipasavyo kutokana na kushambuliwa kwa mizinga.

  Balozi Ma ameongeza kuwa, China inazitaka nchi wajumbe wa Baraza la Usalama zidumishe mshikamanno, kushikilia mwelekeo wa kutatua suala la Syria kwa njia ya kisiasa, na kufikia mpango wa utatuzi unaokubaliwa na pande mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako