• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya kusimamia uchaguzi ya SADC yakutana na waziri wa mambo ya nje wa Zimbabwe

  (GMT+08:00) 2018-03-13 16:46:46

  Timu ya wasimamizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC imekutana na waziri wa mambo ya nje wa Zimbabwe Sibusiso Moyo, wakati ikianza tathmini yake ya wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.

  Akizungumza na timu hiyo, waziri Moyo amesema timu hiyo imefika katika wakati mwafaka, kabla ya mchakato wa uchaguzi haujaanza ili waweze kuelewa na kutoa ushauri wa kiufundi ambao ni muhimu kwa matakwa ya serikali, ya kufanya uchaguzi huru, wa haki na uwazi.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Uchaguzi ya SADC Leshele Thohlane amesema timu hiyo iko nchini Zimbabwe kutathmini hali ya nchi hiyo katika maandalizi ya uchaguzi mkuu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako