• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makubaliano ya kisiasa ya viongozi wa Kenya yaamsha matarajio mema kwa wananchi

  (GMT+08:00) 2018-03-13 16:47:08

  Makubaliano ya kisiasa kati ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mpinzani wake mkuu katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kiongozi wa upinzani Raila Odinga, kumewapa Wakenya matarajio mazuri.

  Viongozi hao walifanya mazungumzo ijumaa iliyopita na kukubaliana kufanya kazi kwa pamoja katika hatua iliyowashtua wafuasi wao na maadui zao, ambao hawakutegemea wakuu hao kushirikiana kutokana na majeraha yaliyotokana na uchaguzi.

  Katika taarifa yao ya pamoja, rais Uhuru na Bw. Odinga wamesema Wakenya wanapaswa kushinda utengano wa kikabila kwa kufanyia kazi uelewa wao kuwa uchaguzi pekee sio suluhisho la changamoto zinazowakabili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako