• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pakistan na Iran kushirikiana kupambana na makundi ya kigaidi ya kuvuka mipaka

  (GMT+08:00) 2018-03-13 16:48:21

  Waziri wa mambo ya nje wa Pakistan Bw. Khawaja Asif amefanya mazungumzo na mwenzake wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif ambaye yuko ziarani nchini humo, na pande mbili zimeeleza kufuatilia hali ya usalama ya Afghanistan, huku zikiona kuwa ni lazima kuimarisha ushirikiano katika kupambana na makundi ya kigaidi ya kuvuka mipaka.

  Taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan imesema, mawaziri hao wawili wamebadilishana maoni kuhusu hali ya usalama wa kikanda na kimataifa, na pande zote mbili zinafuatilia kuwepo kwa kundi la IS nchini Afghanistan na tishio la usalama linaloletwa na kundi hilo kwa ukanda huo. Pia zimesisitiza kuwa nchi hizo mbili zinatakiwa kuimarisha ushirikiano na kupambana na makundi ya kigaidi ya kuvuka mipaka kwa pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako