• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani na Nigeria kushirikiana katika masuala ya usalama

  (GMT+08:00) 2018-03-13 16:48:40

  Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson amesema, nchi hiyo itashirikiana na Nigeria katika masuala ya usalama.

  Bw. Tillerson amesema hayo alipokutana na rais Muhammadu Buhari wa Nigeria mjini Abuja, Nigeria. Rais Buhari amemfahamisha Bw. Tillerson juu ya wanafunzi 110 wa kike waliopotea baada ya kundi la Boko Haram kuvamia shule moja mwezi wa Februari mwaka huu.

  Bw. Tillerson amesema, Marekani inapenda kutoa vifaa vya usalama na kubadilishana habari husika za upelelezi, na pia kutoa mafunzo kwa wanausalama wa Nigeria, ili kuwawezesha kufanya operesheni ya kuwaokoa mateka.

  Mbali na hayo, rais Buhari na Bw. Tillerson pia wamezungumza kuhusu masuala ya uchumi, biashara na uwekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako