• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni za China kutengeneza kivuko kikubwa nchini Algeria

  (GMT+08:00) 2018-03-13 18:56:50

  Kampuni za China na Algeria zimesaini mkataba wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 175 kwa ajili ya kutengeneza kivuko kikubwa nchini Algeria.

  Mkurugenzi wa kampuni ya biashara na ujenzi wa meli ya China (CSTC) tawi la Algeria Bw. Luo Zengqiang amesema, itachukua muda wa miezi 26 kukamilisha utengenezaji wa kivuko hicho, ambacho kitafanya safari kati ya Algeria, Hispania, Italia na Ufaransa.

  Kwenye hafla ya kusaini mkataba huo, waziri wa kazi za umma na uchukuzi wa Algeria Bw. Abdelghani Zaalane amesema, kivuko hicho ni sehemu ya Algeria ya kuongeza uwezo wake wa usafirishaji baharini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako