• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatangaza mpango wa mabadiliko ya Baraza la Serikali

  (GMT+08:00) 2018-03-13 19:21:19

  China imetangaza mpango wa kuvifanyia mabadiliko makubwa vyombo vya Baraza la Serikali unaolenga kufanya serikali iwe na muundo bora, ufanisi zaidi na kuangalia zaidi huduma.

  Mpango huo umewasilishwa kwenye mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China unaoendelea hapa Beijing ili kujadiliwa.

  Baada ya mabadiliko hayo, kutakuwa na Wizara na Kamati 26 zilizo chini ya Baraza la Serikali, ikiwemo Wizara ya Maliasili, Wizara ya Masuala ya Maveterani na Wizara ya Usimamizi wa Dharura.

  Pia kutakuwa na idara mpya kama vile Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Mamlaka ya Uhamiaji ya Taifa, na Kamati ya Usimamizi wa Benki na Bima. Kwa kulinganisha muundo wa sasa wa kamati zilizo chini ya Baraza la Serikali, idara nane za kamati zenye ngazi ya wizara zitaondolewa na saba zenye ngazi ya wizara ndogo zitaondolewa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako