• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuagiza mifuko milioni 6.6 za mahindi kutoka Uganda

    (GMT+08:00) 2018-03-13 19:31:07

    Kenya imeingia katika makubaliano na Kampala kununua mifuko milioni 6.6 ya mahindi kwa Sh2,050 kila mfuko, ili kuziba upungufu ambao umesababisha kupanda kwa bei ya unga.

    Mpango wa mabilion ya shilingi ambao ulipangwa na Wizara ya Biashara utaona wazalishaji wa ndani wakilipa Baraza la Nafaka la Uganda ambayo upeleka mizigo kwa bodi ya Taifa ya nafaka na mazao (NCPB).

    Wafanyabiashara wa ndani, watapata tani 600,000 za mahindi kwa dola 225 kwa kila tani.

    Itasaidia kuziba upungufu wa mifuko milioni tano baada ya hali mbaya ya hewa mwaka jana.

    Mpango wa Uganda unaonekana kuwaumiza wakulima ambao walikuwa wanatarajia kupata faida kutokana na kupanda kwa bei ya mahindi kutoka Sh3,200 hadi Sh3,400 kwa mfuko.

    Uagizaji wa mahindi kutoka Uganda hadi Kenya ulikua kwa asilimia 78 mwezi Januari ikilinganishwa na Desemba 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako