• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Uvuvi haramu waathiri sekta hiyo na mapato yake

  (GMT+08:00) 2018-03-13 19:32:10

  Uzalishaji wa ndani wa samaki, nchini Rwanda unatarajiwa kufikia 30,000 kwa muda mfupi na karibu nusu yake, inatarajiwa kutoka kwa uvuvi wa kawaida.

  Kulingana na Bodi ya Kilimo ya Rwanda (RAB), uvuvi haramu na mbinu kama matumizi ya sumu ya kuua samaki ni changamoto kubwa uzalishaji wa samaki na viumbe hai kwa ujumla.

  John Kubwimana, mwanachama wa KOBOPERATI, shirika la uvuvi, amesema visa vya uvuvi haramu vimeongezeka tangu mwaka jana, na kuumiza uzalishaji wa samaki.

  Rwanda ina uwezo wa kuzalisha tani 200,000, kulingana na mpango wa wakulima wa uvuvi na wa samaki ulioidhinishwa na baraza la mawaziri mwaka 2012.

  Sekta ya uvuvi ilipokea fedha ya bajeti iliyotegewa franc milioni 800 ya mwaka wa fedha 2017/18.

  Lakini kulingana na uchunguzi uliofanywa mwaka 2015 unaonyesha serikali inahitaji kuwekeza angalau franc bilioni 1.5 kila mwaka kwa miaka mitano ili kuongeza uzalishaji wa samaki hadi tani 130,000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako