• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi mwendo kasi Mbagala wapikwa

    (GMT+08:00) 2018-03-13 19:32:28

    Wakati abiria 200,000 wanahudumiwa na Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam kila siku kwa sasa, awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mabasi hayo inayohusisha barabara ya kwenda Mbagala imeanza.

    Tayari Serikali imetangaza zabuni ya ujenzi wa awamu hiyo ambapo waliovutiwa na zabuni hiyo wanatakiwa kuwa na dhamana zenye thamani isiyopungua Sh milioni 480 na kuwasilisha maombi yao kipindi kisichozidi Aprili 10.

    Kwa mujibu wa tangazo la zabuni hiyo lililotolewa baada ya Serikali kupata mkopo kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), mradi utahusisha ujenzi wa jengo la biashara (Mbagala Complex) litakalokuwa na maduka, ofisi za utawala, na kituo cha abiria.

    Mradi kama huu, upo kwenye mataifa mengine matatu ikiwamo Afrika Kusini na Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako