• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AFCON 2018: Twiga Stars yaingia kambini kujiandaa na AFCON, Taifa Stars kuwafuata Algeria wiki ijayo

  (GMT+08:00) 2018-03-14 08:56:18
  Timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) imeingia kambini kujiandaa nmchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake AFCON 2018 yatakayofanyika nchini Ghana.

  Twiga stars itacheza dhidi ya She Polopolo ya Zambia April 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na marudiano April 8 Lusaka Zambia.

  Wakati huo huo, Timu ya Taifa ya wanaume ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki katika kalenda ya FIFA inayoanza Machi 19 hadi 27 mwaka huu, dhidi ya zimu za taifa za Algeria na DR Congo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako