• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michuano ya UEFA Champions League: Manchester United yatupwa nje

  (GMT+08:00) 2018-03-14 08:57:30

  Timu ya Manchester United imetupwa nje la michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora baada ya kuonyesha kiwango kibovu mbele ya Sevilla ya Uhispania na kukubali kichapo cha magoli 2-1 katika uwanja wa nyumbani Old Traford.

  Mabao ya Sevilla yamefungwa na Ben Yedder dakika ya 74 na 78 kipindi cha pili, huku bao la kufutia machozi la Man U likifungwa na Lukaku dakika ya 84.

  Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uhipania, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana. Kwa matokeo hayo yanaiondosha rasmi Man U kwenye michuano hii na inakuwa ni timu ya kwanza toka England kutolewa mashindanoni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako