• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Palestina yalaani shambulizi la mabomu dhidi ya msafara wa waziri mkuu wa nchi hiyo huko Gaza

  (GMT+08:00) 2018-03-14 09:07:37

  Wapalestina wamelaani shambulizi la bomu lililotegwa kando ya barabara dhidi ya msafara wa waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Rami Hamdallah kaskazini mwa ukanda wa Gaza. Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Gaza inasema, bomu moja lililipuka kando ya barabara karibu na mji wa Beit Hanoun, baada ya msafara wa magari ya waziri mkuu kupita katika eneo hilo, na hakuna watu waliojeruhiwa kwenye shambulizi hilo. Ofisi ya rais wa Palestina na maofisa wa chama cha Fatah wamelaani tukio hilo, na kulishutumu kundi la Hamas, ambalo limetawala ukanda wa Gaza tangu mwaka 2007, kuhusika na shambulizi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako