• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapongezwa kwa msaada wake wa kibinadamu kwa Ethiopia

  (GMT+08:00) 2018-03-14 09:18:30

  Shirika la Mpango wa chakula la Umoja wa mataifa WFP na Ethiopia, wamepongeza uungaji mkono wa kibinadamu unaotolewa na China kwa watu walioathiriwa na ukame na wakimbizi nchini Ethiopia.

  Pongezi hizi zimetolewa wakati wa kukabidhi awamu ya nne ya msaada wa kibinadamu uliotokea na China kwenye ofisi WFP mjini Addis Ababa. Msaada huo wenye thamani ya dola milioni 6 za kimarekani utatumika kuwasaidia wakimbizi na waathirika wa ukame nchini Ethiopia.

  Kwa kupitia njia nne tofauti, China mpaka sasa imetoa msaada wa dharura kwa Ethiopia wenye thamani ya dola milioni 36, na kuifanya China kuwa mchangiaji mkubwa wa tatu wa msaada wa chakula kwa Ethiopia.

  Akiongea na wanahabari mjini Addis Ababa, Kaimu mkurugenzi wa WFP nchini Ethiopia Bw. Samir Wanmali, ameishukuru China kwa kuitikia haraka mwito uliotolewa kwa pamoja na WFP na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR kuhusu uungaji mkono kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako