• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maofisa wa nchi za Afrika wataka mbwa wa kunusa watumike katika vita dhidi ya uhalifu wa viumbepori

  (GMT+08:00) 2018-03-14 09:18:50

  Wanamazingira wa nchi za Afrika, watekelezaji wa sheria na maofisa wa forodha, wametoa mwito kwa serikali zao kuwekeza kwa ajili ya mbwa wa kufuatilia na kukamata wanaohusika na biashara haramu ya viumbe pori.

  Wakiongea kwenye kongamano mjini Nairobi, maofisa hao wamesema kuwekwa kwa mbwa kwenye forodha kunaweza kuimarisha kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa watu wanaosafirisha bidhaa zilizopigwa marufuku kama pembe za Tembo na Faru.

  Kaimu mkuu wa shirika la wanyamapori la Kenya Bw Julius Kimani, amesema matumizi ya mbwa waliopatiwa mafunzo, wameimarisha mapambano dhidi ya uhalifu unaohusiana na viumbepori, ambao kwa sasa umekuwa tishio kwa usalama na mazingira ya asili barani Afrika.

  Amesema nchi za Afrika zinatakiwa kutumia mbwa kwenye mapambano yao dhidi ya ujangili ili kuwaokoa Tembo na Faru ambao wako hatarini kutoweka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako