• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu wawataka viongozi wa Kenya kuleta mabadiliko ya kweli baada ya kufikia makubaliano

  (GMT+08:00) 2018-03-14 09:19:08

  Wataalam kwenye jumuiya ya washauri bingwa wamepongeza kufikiwa kwa makubaliano kati ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na kiongozi wa upinzani Bw. Raila Odinga, na kutaka kutumia makubaliano hayo kuleta mabadiliko ya kweli.

  Kundi la International Crisis Group (ICG) limesema umoja ulioahidiwa na viongozi hao unatakiwa kukomesha mgogoro uliotokana na uchaguzi wa rais uliofanyika mwaka jana, kwa kuwa unatoa fursa ya kuwepo kwa majadiliano ya kitaifa, na kuepusha mgogoro kama huo kutokea tena.

  Taarifa iliyotolewa na jumuiya hiyo inasema kipaumbele kinatakiwa kuwa kwenye uchunguzi wa mauaji yaliyofanywa na polisi na kufanya mageuzi ya polisi, kufungua upya taasisi zisizo za kiserikali na vyomba vya habari vilivyofungiwa, mageuzi ya kisiasa ya kuondoa hali ya mshindi kuchukua nafasi zote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako