• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe wa Umoja wa Afrika aitaka Somalia kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi

  (GMT+08:00) 2018-03-14 09:40:26

  Mjumbe maalumu wa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Bw. Fransisco Madeira ametoa mwito kwa majimbo ya Somalia kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi.

  Bw. Madeira amefanya mazungumzo na mkuu wa jimbo la HirShabelle Bw. Mohamed Abdi Waare kuhusu mpango wa kukabidhi jukumu la kulinda usalama kwa kikosi cha kulinda amani cha jimbo hilo, na kusisitiza hitaji la kuharakisha mchakato wa utulivu wa Somalia.

  Bw. Madeira ambaye pia ni kiongozi wa tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM amesema anafahamu changamoto zinazolikabili jimbo la HirShabelle, na kikosi cha kulinda amani kitashirikiana kwa karibu zaidi na jimbo hilo ili kuleta utulivu kwa kuunda taasisi za serikali katika maeneo yaliyokombolewa na AMISOM.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako