• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika la msalaba mwekundu lapanua msaada wa kibinadamu kwa waethiopia wanaokimbilia Kenya

  (GMT+08:00) 2018-03-14 09:40:51

  Shirika la msalaba mwekundu la Kenya limetoa taarifa ikisema hadi kufikia jana waethiopia karibu 5,000, wengi kati yao wakiwa ni wanawake na watoto, wamekimbilia Kenya kutafuta hifadhi, na idadi hiyo huenda ikaongezeka katika siku zijazo.

  Taarifa inasema kwa sasa wakimbizi hao wako katika wilaya ya Moale iliyoko kwenye mpaka wa Kenya na Ethiopia.

  Shirika hilo limefanya tathimini kuhusu hali ya maisha ya wakimbizi hao, na kutoa msaada wa kibinadamu kwao. Kutokana na msimu wa mvua, shirika hilo linakabiliwa na changamoto kubwa za kuhakikisha upatikanaji wa maji safi, usafi wa mazingira na huduma za afya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako