• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya China ya kutengeneza magari ya umeme yasaini makubaliano na UNEP

  (GMT+08:00) 2018-03-14 09:59:59

  Kampuni ya TAILG ya China inayotengeneza magari ya umeme imesaini makubaliano ya ushirikiano na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP, yanayolenga kupeleka magari ya umeme barani Afrika na kwenye maeneo mengine duniani.

  Akizungumza kwenye hafla ya Wiki ya usafi wa hewa ya Afrika mjini Nairobi, Kenya, mkurugenzi wa mauzo wa kampuni hiyo Bw. Xu Rong amesema, makubaliano hayo yatasaidia serikali za nchi za Afrika kusitisha hatua kwa hatua matumizi ya magari yanayochafua mazingira ili kupunguza uchafuzi wa hewa.

  Bw. Xu amesema ushirikiano huo pia utakuwa na mafunzo, ambayo baadhi ya maofisa wa serikali za nchi za Afrika watatembelea makao makuu ya kampuni yao nchini China na kujifunza kuhusu mambo ya magari hayo. Pia amesema, kampuni yao itaendelea kufanya utafiti kuhusu mambo ya mazingira na usafiri barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako