• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • OPCW laipongeza Iraq kuteketeza silaha zote za kikemikali

  (GMT+08:00) 2018-03-14 10:01:43

  Shirika linalopiga marufuku silaha za kikemikali OPCW jana kwenye makao makuu yake huko The Hague nchini Uholanzi lilitoa taarifa kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw. Ahmet Uzumucu ameipongeza Iraq kutokomeza silaha za kemikali kwa pande zote.

  Taarifa hiyo imesema Bw. Uzumucu siku hiyo alipokutana na ujumbe wa serikali ya Iraq alisema anakaribisha mafanikio hayo. Serikali ya Iraq imefanya juhudi kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Mkataba wa kupiga marufuku silaha za kikemikali na kuhakikisha silaha zote za kikemikali nchini humo zinateketezwa.

  Taarifa imethibitisha kuwa viwanda vinne vya kutengeneza silaha za kikemikali nchini Iraq vimeteketezwa kikamilifu, na kiwanda kingine kilichotumiwa kutengenezwa silaha hizo kilirekebishwa kwa ajili ya matumizi yanayoruhusiwa na Mkataba wa Kupiga marufuki Silaha za kikemikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako