• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanawake wa Sudan Kusini wataka ushiriki zaidi katika mchakato wa kurejesha amani

  (GMT+08:00) 2018-03-14 10:29:04

  Wanawake wa Sudan Kusini wametaka kuwa na ushawishi zaidi katika raundi ya tatu ya mazungumzo ya kurejesha amani yatakayofanyika hivi karibuni nchini Ethiopia.

  Naibu waziri wa habari Bibi Lily Albino amesema wanawake wanapaswa kushiriki zaidi katika Baraza la ngazi ya juu la ustawishaji HLRF litakalofanyika mwezi Machi kupitia Shirika la maendeleo ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD nchini Ethiopia.

  Bibi Albino akihutubia ufunguzi wa mafunzo ya amani kwa wanawake yaliyoandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNMISS amesema, wanawake wanadai kuongeza uwakilishi wake katika baraza hilo kutoka asilimia 25 hadi kufikia asilimia 50 kwa mujibu wa makubaliano ya mwaka 2015. Aliongeza kuwa pia wanataka kuwa na uwakilishi wa asilimia 35 katika mkutano wa mazungumzo ya kitaifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako