• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la Afghanistan lawakamata wapiganaji wanne akiwemo kiongozi muhimu wa Taliban

  (GMT+08:00) 2018-03-14 17:44:19

  Msemaji wa jeshi la Afghanistan Bw. Nasratullah Jamshidi amesema, jeshi hilo limewakamata wapiganaji wanne akiwemo kiongozi muhimu wa kundi la Taliban Qari Abkhtiar kwenye mapambano dhidi ya wapiganaji wa kundi hilo nje ya Pul-e-Khumri, mji mkuu wa mkoa wa Baghlan, kaskazini mwa nchi hiyo.

  Bw. Jamshidi amesema, Qari Abkhtiar alishughulikia mipango ya kutega mabomu barabarani na kuwashambulia maofisa wa usalama kwenye mkoa wa Baghlan, na kukamatwa kwake ni pigo kubwa kwa kundi la Taliban.

  Habari nyingine zinasema, maofisa wawili wa polisi wa Afghanistan wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kwenye shambulizi la bomu lilotegwa kwenye gari dhidi ya kituo cha ukaguzi cha polisi mpakani mkoani Helmand, kusini mwa nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako