• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Madai ya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya walinzi amani wa Umoja wa Mataifa yapungua mwaka jana

  (GMT+08:00) 2018-03-14 18:19:15

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, mwaka jana walipokea madai 62 ya udhalilishaji wa kijinsia unaofanywa na walinzi amani wa Umoja huo dhidi ya raia wa kawaida, idadi ambayo ilipungua sana ikilinganishwa na madai 104 kama hayo mwaka juzi.

  Ripoti iliyotolewa na Katibu Mkuu huyo imesema, mwaka jana Umoja huo ulipokea madai 138 ya dhuluma na udhalilishaji wa kijinsia yanayohusiana na wafanyakazi wasiotoka vikosi vya Umoja wa Mataifa walioidhinishwa na ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, ujumbe wa siasa na mashirika mengine ya Umoja huo, 62 kati yao yakihusiana na walinzi wa amani wa Umoja huo.

  Ripoti hiyo pia imesema, ili kupunguza vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa raia wa kawaida, Umoja huo umechukua hatua nyingi kuimarisha ukaguzi kabla ya kuwaajiri walinzi hao na kutoa mafunzo kwa walinzi hao kabla na baada ya kupelekwa katika sehemu husika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako