• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kufanya juhudi pamoja na waziri mpya wa mambo ya nje wa Marekani ili kuendeleza uhusiano kati ya pande mbili

    (GMT+08:00) 2018-03-14 18:33:53

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, China inapenda kufanya juhudi pamoja na waziri mpya wa mambo ya nje wa Marekani ili kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Donald Trump wa Marekani jana alitangaza kumwondoa Bw. Rex Tillerson madarakani na kumteua Mike Pompeo aliyekuwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi ya CIA kuwa waziri mpya wa mambo ya nje wa nchi hiyo.

    Bw. Lu amesema, China inapenda kufanya juhudi pamoja na waziri huyo mpya kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili, hatua ambayo inaendana na maslahi ya watu wa pande mbili na matarajio ya jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako