• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Bei za maziwa zatarajiwa kushuka msimu wa mvua unapoanza

    (GMT+08:00) 2018-03-14 19:25:39

    Wakati mvua zikiendelea kushuhudiwa sehemu mbalimbali za Afrika Mashariki,wadau katika sekta ya maziwa nchini Uganda wanatarajia bei za maziwa na bidhaa za maziwa kushuka.

    Kilimo nchini Uganda,ikiwa na pamoja na kilimo cha mifugo ya maziwa,hutegemea sana mvua za msimu.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Maendeleo ya Kilimo cha Maziwa Dk Jolly Zaribwende amesema mwanzo wa mvua unaashiria sio tu uzalishaji wa chakula na nyasi kwa kiwango kikubwa,lakini pia afueni kwa mifuko ya wateja.

    Kwa sasa bei ya maziwa lita moja ni kati ya Sh1,100 and Sh1,200.Lita moja maziwa ambayo hayajasindikwa ni Sh1,600 au Sh1,800,wakati lita moja ya maziwa yaliyosindikwa ikiuzwa kwa kati ya Sh2,800 na Sh3,000, kulingana na kampuni.

    Zaribwende anasema kama bidhaa nyenginezo za kilimo,wakati kukiwa na mavuno ya kutosha inamaanisha bidhaa hiyo itapatikana kwa wingi.

    Aliongeza kuwa mvua zikiwa za kutosha kutakuwa na maziwa mengi na hivyo bei ya maziwa itapungua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako