• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Deni la taifa (Sh.trilioni 47.756) lipo chini ya kiwango cha hatari,asema waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango

    (GMT+08:00) 2018-03-14 19:28:10

    Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania Dk Philip Mpango amesema kuwa deni la Taifa hadi kufikia Desemba mwaka jana ni Sh.trilioni 47.756 na kwa tathmini iliyofanyika deni hilo lipo chini ya kiwango cha hatari.

    Dk Mpango alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akiwasilisha kwa wabunge mapendekezo ya serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa nay a kiwango na ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2018/2019.

    Alisema kuwa kati ya kiasi hichoi,deni la nje ni Sh.trilioni 34.148 ikiwa ni asilimia 71.5 ya deni lote.

    Aidha alisema deni la ndani lilikuwa Sh.trilioni 13.607 sawa na asilimia 28.5 ya deni hilo.

    Alisema tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika mwezi Novemba 2017 kwa kipindi kilichoishia Juni 2017,inaonesha kuwa deni ni himilivu kwa kipindi cha muda wa kati na mrefu.

    Hata hivyo alsiema uwiano wa deni la ndani nan je kwa pato la taifa kwa mwaka 2017/18 ni asilimia 34.4 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 56,hivyo deni bado lipo chini ya kiwango cha hatari.

    Aliongeza kuwa uwiano wa deni la nje na mauzo ya nje ni asilimia 81.1 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 150.Alisema kuwa uwezo wa taifa kulipa deni hilo bado ni imara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako