• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Rwanda umekua kwa asilimia 6.1 mwaka 2017

    (GMT+08:00) 2018-03-14 19:29:58

    Ukuaji wa uchumi wa Rwanda umepitiliza matarajio ya ukuaji wa asilimia 5.2 na kukua kwa asilimia 6.1 mwaka jana,utendaji mzuri ambao haswa umesababishwa na ukuaji katika robo ya nne ya mwaka.

    Takwimu zilizotolewa jana na Taasisi ya Taifa ya Takwimu Rwanda zinaonyesha kuwa katika mwaka 2017 pato la taifa lilikadiriwa kuwa Rwf7,597 bilioni kutoka Rwf6,672 bilioni mwaka 2016.

    Uchumi ulikua kwa asilimia 6.1 mwaka 2017 ,ukuaji huo ukichangiwa pakubwa na kilimo,viwanda,na huduma ambazo zilichangia asilimia 31,16,na 47 mtawalia.

    Nchi hiyo ilikuwa na utendaji mbaya katika robo ya kwanza nay a pili mwaka 2017,ukuaji wa mwaka hasa ulichangiwa na ukuaji katika robo ya nne ya mwaka ambao ulikuwa asilimia 10.5.

    Waziri wa Fedha na Upangaji Uchumi,Balozi Claver Gatete, amewapongeza wanyarwanda kwa ukuaji huo wa uchumi ,na kusema kuwa ni jambo zuri kuwa ukuaji wa mwaka 2017 umepita makadirio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako