• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka-Klabu Bingwa Ulaya, Barcelona yafuzu robo fainali kwa kuifunga Chelsea 3-0, Messi ang'ara, afikisha magoli 100

    (GMT+08:00) 2018-03-15 08:43:46

    Nyota Lionel Messi amefunga magoli mawili muhimu katika ushindi wa 3-0 dhidi ya timu ya Chelsea, yaliyoifanya timu yake ya Barcelona ifuzu robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa ulaya.

    Magoli hayo mawili yamemfanya Messi afikishe jumla ya magoli 100 aliyofunga katika michuano hiyo.

    Kwa ushindi huo Barcelona sasa inafuzu robo fainali ya klabu bingwa kwa mara ya 11 mfululizo, na hiyo ikiwa ni mara yake ya 15 kuwahi kufuzu robo fainali.

    Katika mechi hiyo iliyofanyika jana, Messi alifunga goli la kwanza kwa timu yake dakika ya 3 na goli la tatu kunako dakika ya 63, huku goli la pili la timu hiyo likifungwa na Ousmane Dembele katika dakika ya 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako