• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kriketi-Rwanda, Martin Suji wa Kenya atangazwa kuwa kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Wanaume ya Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-03-15 08:44:39

    Martin Suji kutoka Kenya ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Rwanda ya mchezo wa Kriketi wanaume, kwa mkataba wa miezi minne.

    Akimtangaza Suji, Rais wa Chama cha Kriketi cha Rwanda RCA, Eddie Balada amesema anaanza rasmi kazi mwezi huu akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Davis Turinawe wa Uganda na jukumu lake kuu ni kuiandaa timu kwa ajili ya mechi za kufuzu mashindano ya dunia kwa mwaka 2019 zitakazofanyika mwezi juni mwaka huu.

    Rwanda ndio wenyeji wa mechi za kufuzu kombe la dunia ngazi ya kanda ambapo itazikaribisha timu kutoka Tanzania, Uganda na Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako