• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Nyumba zilizojengwa ovyo zajunjwa Nairobi

    (GMT+08:00) 2018-03-15 20:52:53

    Shughuli ya kubomoa majengo duni jijini Nairobi itarejelewa Alhamisi wiki hii katika mtaa wa Huruma ambako majengo 12 yatabomolewa.

    Shughuli hiyo ilisitishwa mwaka uliopita kutokana na ukosefu wa pesa. Kaimu mkurugenzi wa taasisi kuhusu ubora na usalama wa majengo Samuel Charangu alisema kuwa shughuli hiyo itaanzia mitaani Huruma na Zimmerman mara tu idara hiyo itakapopokea fedha.

    Katibu mkuu wa kitaifa wa idara ya majengo aliye pia soroveya mkuu wa serikali Moses Nyakiongora alisema kuwa majengo hayo yalijengwa kwenye maeneo ya mito na yale chepechepe. Charangu alisema kuwa takriban majengo 40 katika mtaa wa Pipeline yalipatikana yasiyo thabiti na yanahitaji kuhimiliwa.

    Wajenzi walipewa muda wa siku saba kufanya hivyo la sivyo serikali itayabomoa. Charangu alisema kuwa wakaguzi wa majengo wamepelekwa kwenye mtaa wa Kariobangi pamoja na maafisa wa kaunti ya Nairobi ambako jengo la orofa nne liliporomoka wakati wa mapambazuko siku ya Jumamosi huku familia kadhaa zikiachwa bila makazi.

    Maafisa wa idara ya ukaguzi wa majengo wanakagua majengo zaidi katika eneo hilo kubainisha uthabiti wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako