• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yajikongoja kwa nafasi moja katika viwango vya soka vya FIFA

    (GMT+08:00) 2018-03-16 09:05:14

    Taifa la Kenya limefanikiwa kupanda kwa nafasi moja katika orodha ya iliyotolewa jana na FIFA, ya ubora wa soka katika mataifa yote ulimwenguni. Awali, Kenya ilikuwa ikishikilia nafasi ya 106, ilivuka hadi nafasi ya 105 nyuma ya majirani zao Uganda iliyoko katika nafasi ya 78. Katika orodha hiyo ya FIFA iliyotolewa hakuna taifa lolote barani Afrika lililopata nafasi kwenye kundi la kwanza la mataifa 20, Tunisia ikiorodheshwa kama timu bora zaidi barani Afrika ikiwa katika nafasi ya 23, haikusonga. Mataifa mengine yaliyoonekana kupepea barani Afrika ni pamoja na Senegal (27), Demokrasia ya Congo (39), Morocco (42), Misri (44), Cameroon 51, na Nigeria 52. Tanzania ipo katika nafasi ya 146 ulimwenguni. Kwa ulimwenguni, Ujerumani inaongoza ikifuatwa na Brazili, kisha Ureno na Argentina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako