• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AFC Leopards yasitisha mkataba wa kocha Robert Matano

    (GMT+08:00) 2018-03-16 09:05:32

    AFC Leopards imemfuta kazi kocha Robert Matano baada ya wakuu wa klabu hiyo kusitisha mkataba wake jana, Machi 15 baada ya kuweka rikodi ya matokeo mabaya kwenye ligi ya KPL. Kwa sasa, Kocha msaidizi Dennis Kitambi atachukuwa nafasi ya Matano kama kocha wa muda huku klabu hiyo ikiendelea kumtafuta mrithi wa kocha huyo. Kwa mujibu wa katibu wa AFC Leopards Timothy Lilumbi, mkataba wa Matano umesitishwa tu na sio barua ya kumfukuza kazi.

    Matano alikuwa amekwisha pewa ilani ya miezi miwili ya kusitishwa kwa mkataba wake kutokana na matatizo ya nidhamu na uhusiano wake na wachezaji. Msimu uliopita, Ingwe ilipata matokeo mabaya na kumaliza msimu ikiwa nafasi ya 11 kwenye ligi ya KPL.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako