• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabondia wa Tanzania watakaoshiriki michezo ya Jumuiya ya Madola 2018 wajiandaa vyema

    (GMT+08:00) 2018-03-16 09:05:50

    Mabondia watakaobeba bendera ya Taifa kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola 2018 wamejazwa 'upepo' na kocha wa timu hiyo Benjamin Oyombi. Kocha huyo Mkenya ambaye atakwenda na timu yake Australia, alisema maandalizi ya mabondia hao wa ridhaa yamekuwa na mafanikio.

    Oyombi alisema ana matumaini mabondia hao watatoa upinzani mkali katika michezo ya Madola iliyopangwa kuanza Aprili 4 mpaka 15 katika mji wa Gold Coast. Ngumi ina rekodi ya kuiletea Tanzania medali tano za Madola zilizotwaliwa na Michael Yombayomba ambaye ni bondia pekee aliyeshinda dhahabu mwaka 1998 mjini Kuala Lumpur Malaysia.

    Mabondia wengine ni Willy Isangura (shaba), Haji Ally (fedha), Bakari Mambeya (shaba) na Hassani Matumla (shaba). Mbali na ndondi pia Tanzania itawakilishwa na wanariadha, waogeleaji na wachezaji wa tenisi ya meza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako