• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pato la kampuni ya ZTE lafikia dola za kimarekani bilioni 17 mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-03-16 16:47:41

    Ripoti iliyotolewa jana na Kampuni ya mawasiliano ya simu ya China ZTE imesema, kampuni hiyo imepata pato la dola za kimarekani bilioni 17.2 mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.5 ikilinganishwa na mwaka 2016.

    Ripoti hiyo imesema ZTE imewekeza kiasi cha dola za kimarekani bilioni 2 katika utafiti na maendeleo, ikiwa ni karibu asilimia 12 ya pato la jumla. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka jana, kampuni hiyo ilikuwa na wafanyakazi elfu 29 wa kufanya utafiti, ambao ni karibu ya asilimia 40 ya wafanyakazi wote wa kampuni hiyo.

    ZTE ni kampuni inayoongoza duniani kwa kutoa vifaa vya mawasiliano, utatuzi wa masuala ya mtandao, na moja ya kampuni zinazokua kwa kasi duniani katika utengenezaji wa simu za kisasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako