• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaendelea kutekeleza sera ya maendeleo ya elimu inayolenga zaidi mahitaji ya jamii

    (GMT+08:00) 2018-03-16 17:48:38

    Waziri wa Elimu wa China Bw. Chen Baosheng amesema katika miongo kadhaa iliyopita, China imepiga hatua kubwa zaidi katika utoaji wa elimu na kufikia nafasi za juu katika viwango vya ubora wa elimu.

    Amesema mpango wa serikali ni kutekeleza mkakati wa kuongeza ubora wa elimu kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu, jambo ambalo limepata mafanikio makubwa katika miaka iliyopita.

    Katika mpango huo, waziri Baosheng amesema mara kwa mara serikali imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa utoaji wa elimu katika taasisi zote za elimu nchini, kwa kupima mitaala inayotolewa pamoja na uwezo wa ufundishaji wa walimu. Amesema elimu ya China inazingatia mahitaji ya jamii ili kuboresha maisha ya watu, hivyo ni muhimi kujitathmini na kuhakikisha kuwa inakuwa na manufaa kwa wananchi na kupima ufanisi wake katika hatua ya utekelezaji.

    Katika hatua nyingine, waziri Baoshen amesema moja ya kipaumbele cha serikali inayoongozwa na Rais Xi Jinping, na ikiwa ni kwa mujibu wa mapendekezo ya mwelekeo uliotolewa na CPC, ni kudumisha ushirikiano mwema na nchi za nje. Elimu ya juu ni moja ya sekta zilizopo kwenye mikakati hiyo ikiwemo mahusiano baina ya vyuo vikuu vya nchini China na vile vya nchi zingine. Amesema katika kutimiza hilo, China inajifunza sera na mifumo mbalimbali ya kuboresha elimu, mitaala na namna za ufundishaji kutoka vyuo vya nje ili kupata viwango vya juu vya ubora wenye kuheshimika wa elimu unaotakiwa. Amesema kwa upande wa elimu, milango ya ushirikiano baina ya taasisi za elimu imeimarishwa sana, na mkakati huu umelenga zaidi kunufaishana kwa pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako