• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jukwaa la fursa za biashara Zanzibar

    (GMT+08:00) 2018-03-16 20:07:57

    Jukwaa la fursa za biashara Zanzibar linafanyika leo kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi mjini Unguja. Jukwaa hilo lililoandaliwa na kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) litawezesha kuzitangaza na hatimaye kufahamika kwa fursa zaidi visiwani humo kwa kuwa si zote zinazofahamika.Jukwaa hilo ni la tano tangu TSN ianze kuandaa majukwaa hayo na ni la kwanza Zanzibar.

    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa Bodi ya TSN, Hab Mkwizu wanatarajiwa kuhudhuria jukwaa la Zanzibar.

    Jukwaa la kwanza lilifanyika Februari mwaka jana mkoani Simiyu, likafuatiwa na la Mwanza, Tanga na Shinyanga. Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo anasema, jukwaa hilo ni muhimu si tu kibiashara bali pia kukuza mahusiano na undugu baina ya wananchi wa Tanzania bara na Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako