• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Putin wa Russia amtumia pongezi Bw. Xi Jinping kuchaguliwa kuwa rais wa China

    (GMT+08:00) 2018-03-17 11:34:45
    Rais Vladimir Putin wa Russia amemtumia salamu za pongezi Bw. Xi Jinping kutokana na kuchaguliwa kwake kuwa rais wa China kwa awamu nyingine.
    Kwenye salamu za pongezi, rais Putin amesema kuchaguliwa kwa Bw. Xi Jinping kunaonesha kwa mara nyingine heshima yake kubwa, na pia kumsifu kwa mchango wake kwa ajili kuhimiza maendeleo ya kasi ya uchumi na jamii ya China, na kulinda maslahi ya China kwenye jukwaa la kimataifa.
    Rais Putin pia amesema anatarajia kushirikiana zaidi na rais Xi Jinping kwenye kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya Russia na China, ili kukuza urafiki na maslahi ya watu wa nchi zao, na pia kuhimiza usalama na utulivu wa Bara la Ulaya na Asia na dunia nzima.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako