• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajumbe wa Bunge la Umma la China watoa mapendekezo kwa hatua za kulenga za kuondoa umaskini

    (GMT+08:00) 2018-03-19 16:41:47

    Kwa mujibu wa ripoti ya kazi ya serikali iliyotolewa mwaka huu, China itaongeza nguvu za kuondoa umaskini kwa hatua zinazowalenga watu kwa usahihi. Kwenye mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China unaoendelea hapa mjini Beijing, wajumbe wametoa mapendekezo yao kuhusu kazi hiyo.

    Qin Yuefei aliyezaliwa mwaka 1988 na kuhitimu kwenye chuo kikuu cha Yale nchini Marekani ni msimamizi wa kijiji kimoja cha mlimani pembezoni mwa mkoa wa Hunan, kusini kati mwa China. Katika miaka sita iliyopita, aliongozana na wanavijiji kuboresha mfumo wa usambazaji wa maji, kujenga nyumba kwa ajili ya wazee, kuinua mwamko kuhusu usalama wa magari ya shule kijijini ,na kufikisha internet ya WIFI shuleni. Hatua hizo zimeleta mabadiliko makubwa kwa sura na maisha ya wakazi wa kijiji hicho. Akitumia mfano wa ushiriki wake kwenye mradi wa kuondokana na umaskini, kijana huyu amependekeza kukamilisha mfumo wa huduma ili kuwavutia vijana zaidi wenye ujuzi kwenda vijijini. Anasema,

    "Vijana wenye uvumbuzi wakija vijijini, sio tu wanaweza kupata msaada wa serikali kwa ajili ya miradi ya kuwasaidia watu maskini, bali pia makampuni maarufu na wajasiriamali na wawekezaji bora wanapenda kutoa ufundi stadi au raslimali. Katika miaka kadhaa ijayo, vijana wenye uvumbuzi wanaojihusisha kwenye miradi ya kuwasaidia watu maskini sio tu wanaweza kuchangia juhudi za serikali za kuondoa umaskini, uwezo wao pia utaweza kuinuka, na kuwa na nafasi zaidi katika soko la ajira, hatimaye kutakuwa na hali ambayo kijana atapenda, kuweza kukaa, kufanya kazi vizuri vijijini na pia vijana wapya watakuja na kuendelea na kazi zao."

    Ili kufanikisha hatua zinazowalenga watu kwa usahihi ili kuwaondoa kwenye umaskini, kampuni ni muhimu. Mjumbe wa Bunge kutoka mkoa wa Shandong Sun Peishu amependekeza kutumia Big Data kutambua kwa usahihi, kuwalenga watu kwa usahihi na kutathmini matokeo kwa usahihi.

    "Kujumuisha teknolojia ya Big Data kwenye kazi za kuwasaidia watu maskini kunaweza kujua idadi halisi ya watu maskini, sababu ya umaskini, kutekeleza ipasavyo hatua za kuwasaidia watu maskini, na kufikisha nyumbani sera za kuwasaidia watu maskini, na kushinda vita dhidi ya umaskini."

    Katika miaka mitano iliyopita, watu milioni 68 wameondokana na umaskini nchini China, yaani kila mwaka watu milioni 13.7 wanaondokana na umaskini, na kiwango cha kutokea kwa umaskini kimepungua kutoka asilimia 10.2 hadi asilimia 3.1. Ifikapo mwaka 2020, watu wote maskini vijijini wanatarajiwa kuondokana na umaskini kwa mujibu wa kigezo cha sasa. Ripoti ya kazi ya serikali ya mwaka huu imebainisha kuwa mwaka huu watu wengine zaidi ya milioni 10 wataondokana na umaskini, na watu milioni 2.8 watahamishwa kutoka kwenye makazi duni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako