Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tantrade, Edwin Rutageruka alisema hayo aliposhiriki katika mjadala wa Jukwaa la Fursa za biashara Zanzibar.
Aidha alisema mwishoni mwa mwaka huu, wanatarajia kwenda nchini Afrika Kusini na Kenya katika biashara na uwekezaji wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Muungano.
Amesema kwa sasa (TanTrade), wanaweka mkakati katika kuongeza thamani ya mazao kama mwani ambao unaweza kuzalisha zaidi ya bidhaa 46 na kuacha kusafirisha zikiwa hazina thamani na kuuzwa kwa Sh 500 kwa kilo.
Rutageruka alisema wanatarajia kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa hizo ikiwemo sabuni na kwamba watahakikisha watalii wanaoingia visiwani humo wanatumia bidhaa na kusaidia kutoa ajira na kukuza uchumi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |