• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yafuatilia uchaguzi wa viongozi wa awamu mpya wa serikali ya China

    (GMT+08:00) 2018-03-20 09:46:08

    Jumuiya ya kimataifa inafuatilia viongozi wa awamu mpya wa serikali ya China waliochaguliwa kwenye Mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China, wakiona China itaendelea kutoa mchango kwa maendeleo ya uchumi wa dunia na usimamizi wa mambo ya dunia.

    Profesa John Smith wa Kitivo cha siasa za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Midrand cha Afrika Kusini, anaamini kuwa viongozi wa awamu mpya wa serikali ya China watakuwa na uwezo wa kutatua masuala ya kutokomeza umaskini, kudhibiti uchafuzi wa mazingira na kutimiza maendeleo yasiyo na uchafuzi wa mazingira. Pia anatumai kuwa China itaendelea kuzisaidia nchi za Afrika kupata maendeleo ya pamoja.

    Mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya mahusiano ya kidiplomasia na mikakati ya Ethiopia Bw. Abebe Enet ana matumaini kwamba viongozi wa awamu mpya wa serikali ya China wataiongoza China kuimarisha ushirikiano na mashirika ya kikanda na ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, na kuchukua nafasi muhimu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako