• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China aahidi kufungua zaidi soko la China

    (GMT+08:00) 2018-03-20 16:27:48

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang amesema nchi hiyo itafungua zaidi soko lake kwa dunia.

    Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa Mkutano wa Bunge la Umma la China hii leo, Bw. Li amesema uchumi wa China umeingiliana sana na uchumi wa dunia kiasi kwamba kufunga mlango kutazuia tu njia ya China. Amesema China bado ina nafasi kubwa ya kuendelea kufungua soko lake, na itapunguza ushuru kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo.

    Waziri mkuu huyo amesema licha ya upungufu kwenya biashara ya huduma, China itaongeza juhudi katika kulegeza udhibiti wa upatikanaji wa soko katika sekta ya huduma, ikiwemo huduma kwa wazee, huduma za afya, elimu, na huduma za kifedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako